Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally aukubali mziki wa Yanga

Yanga Azam F Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao dhidi ya Azam FC.

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Simba umeweka wazi kuwa utadhihirisha ukubwa wao kwa kupata ushindi kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni Kariakoo Dabi inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 kwa timu zote kuwania kupata pointi tatu muhimu.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa wanatambua ushindani utakuwa mkubwa na wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mchezo huo.

"Azam hawezi kutufikia tena, mpinzani aliyebaki ni Yanga ambaye na yeye tunataka kumfunga na kumpita kwa alama sita. Ni mechi ambayo tunaitaka kweli kweli, kuanzia kwa mashabiki, benchi la ufundi, wachezaji na viongozi ndio hata hatulali,"

Ndivyo alivyonukuliwa Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally katika Mkutano wake na wanahabari kuelekea mchezo wao wa ‘Kariakoo Derby’ watakapomenyana dhidi ya kikosi cha Yanga kuwania ubingwa Ligi Kuu Tanzania.

"Tumewekeza zaidi kwenye kuwafurahisha mashabiki wetu, Jumapili ya Novemba 5, 2023 tunataka kuwafurahisha. Na anayeshinda mchezo huo ndio atatawala nchi hadi tukikutana tena," amesema Ahmed.

Amesema "Tumecheza mechi ngumu lakini mechi ya Jumapili ni ngumu kuliko zote hii ni kutokana na utani uliopo pamoja na ubora wa timu yao. Tunaona namna wachezaji wao wanajituma. Mechi yetu dhidi yao ni ngumu kweli kweli, mechi ya kipimo cha mpira wa nchi haiwezi kuwa nyepesi."

Aidha, kiongozi huyo amewaasa mashabiki wa klabu hiyo kijitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwapa nguvu wachezaji wao, sambamba na hayo amewaasa kuwa watiifu kwa kuzingatia kampeni ya kuhamasisha vitendo vya kiungwana michezoni ‘Fair play’.

"Mashabiki wetu tuzingatie misingi ya uungwana na ustaarabu, tujitahidi tushangilia na kutaniana kwa heshima ili kuepusha vurugu. Tuendeleze Utanzania kwa utu na upendo," amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: