Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally anaingizwa chaka na viongozi timu mbovu ile - Shabiki wa Simba

Viongozi Wa Simba 32674 Viongozi wa Simba

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba maarufu kwa jina la Miraji amesema kuwa viongozi wa timu hiyo wamemwachia Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahemd Ally huku wao wakiendelea na mambo yao binafsi.

Miraji amesema kuwa si Mwenyekiti wa Klabu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CEO wa Klabu ambaye kwa sasa yupo karibu na timu kwani wamekwenda Dubai kufanya shopping za sikukuu na wamemwachia Ahmed afanye kila kitu jambo ambalo linaifanya timu isipate matokeo chanya uwanjani.

“Timu imetoka Misri hakuna kiongozi hata mmoja aliyerudi na timu, wote walienda Ulaya na wengine Dubai kufanya shopping za sikukuu, timu imeondoka na Ahmed Ally na Abbas Ally hakuna kiongozi yeyote zaidi ya hao, unaenda kucheza na mashujaa unadhani utashinda?

“Ahmed Ally afanye hamasa, aingie kwenye kamati ya ushindi, yani anafanya kazi zaidi ya tatu. Angekuwa msemaji wa timu nyingine angekuwa ameshafungiwa yule jamaa. Ahmed Ally ndiye amebaki faraja yetu pekee maana matokeo ni mabovu. “Yeye wanamuingiza chaka, anaona kabisa timu ni mbovu haina maanadlizi ila anawaaminisha mashabiki njooni timu itafanya vizuri, sisi atatuchukia bure, unaifagiliaje timu haina maandalizi.

“Unakuja kutuambia Simba ni bora watu wanaongea sana, mimi nauliza Mashujaa nao wanadhaminiwa na Hier? Kila tunapofungwa tunatafuta gape la kutokea sababu viongozi wetu wameshajua mashabiki wengi wa Simba wanapenda kupumbazwa kwa vitu ambavyo havina maana.

“Timu inaenda Misri kucheza mchezo mgumu na Al Ahly halafu viongozi wakashikilia bango kwamba Yanga inapendelewa sijui Simba hawajapewa pesa kusafirisha mashabiki zao, hii yote ni viongpozi kuficha madudu yao na sisi mashabiki tukaingia mkumbo.

“haikuishia hapo wakatuongeza kitu cha pili cha Mayele, tumzungumzie Mayele, sasa kutusahaulisha kipigo cha Mashujaa watupe part 2 ya Mayele. Kama waliweza kutuletea Manzoki kwenye uchaguzi badala ya usajili… ile interview mayele wamemlipa pesa ndefu tu.

“Tusiongopeane, tuna asilimia chache mno za kwenda kuchukua ubingwa wa ligi na kama msimu huu Simba atachukua Ligi yatakuwa maajabu ya mpira wa nchi hii. Kwa kikosi kile, maandalizi yale na uchezaji ule, itakuwa maajabu?

“Timu inapangwa kuangalia nani mwenye bahati, leo muweke Pa Omary Jobe, akishindwa basi tuangalie Fredy Michael kama atakuwa na bahati leo, yani inabidi tucheke ili tujifariji,” Miraji.

Simba kwa sasa inapitia wakati mgumu baada ya hivi karibuni ikiondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuondoshwa pia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania na jana kutoa sare dhidi ya Ihefu kwenye mchezo wa ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live