Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally anaichukulia poa Ruvu Shooting

Ahmedally  20220121 0001 Ahmed Ally anaichukulia poa Ruvu Shooting

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Furaha ya ushindi dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast bado imeendelea kushamiri kwa Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally, licha ya kikosi cha klabu hiyo kukabiliwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi Ruvu Shooting leo Jumatano (Februari 16).

Ahmed Ally ambaye furaha yake ilianza baada ya ushindi wa 3-1, Jumapili (Februari 13), ameonesha kuendelea kuwa katika hali hiyo kufuatia andiko lake kwenye mtandao wa Instagram.

Ahmed amethibitisha kuwa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kwao ni kama sehemu ya kuweka mwili sawa, huku wakijiandaa na mpambano wa pili wa hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendermerie ya Niger.

“Tarehe 16 ni mechi ya kurifresh kidogo kwa ajili ya kurejesha mwili sawa wakati huo tukijiandaa na mechi inayaofuata dhidi ya Gendermerie huko ndiko Simba tunaonjoy kucheza.”

Simba SC itacheza dhidi ya US Gendermerie nchini Niger Jumamosi (Februari 20).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live