Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally amtetea kipa Abel "Asilaumiwe"

Ahmed Simba Msz Ahmed Ally na Abel

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasilino Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo hawapaswi kumlaumu kipa wao, Hussein Abel kwa kosa alilolifanya la kudaka mpira kisha akauangusha kwenye boksi na kusababisha kufungwa bao la mapema na Geita Gold FC kwa shuti la Geofrey Julius dakika ya 10 tu kwenye mchezo wao wa jana.

Ahmed amesema hayo baada ya kutamatika kwa mchezo huo ambao licha ya kutanguliwa kufungwa, Simba walifanikiwa kushinda mchezo huo wa Ligi kwa mabao 4-1 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

“Nimefurahi Abel Hussein kufanya lile kosa kwa sababu linamkomaza, yaani katika maisha yako yapende zaidi makosa yako kuliko mazuri kwa sababu makosa yako yanakufanya kuwa bora. Kosa alilolifanya uhakika ni kwamba hatolifanya tena katika michezo inayokuja, maana yake anazidi kuimarika.

“Namna ambavyo aliufuata ule mpira maana yake siku nyingine mpira kama ule ukija atakumbuka nilifanya kosa ataongeza umakini, aidha ataupangua ama atakaza mikono kuukamata. Kwa hiyo alivyofanya lile kosa nilisema ‘YES’ hasa ni muda wa Abel Hussein kupatia.

“Kwa hiyo sio kosa la kumlaumu ni kosa la kumkomaza, na watu wote bora duniani wamepitia makosa makubwa ndio maana wamekuwa bora, kwa hiyo kwa Abel Hussein kile ambacho amekifanya kinamuongezea thamani sasa. Na huyu ni Kipa ambaye tunamtegemea mno kwa msimu ujao, kwa hiyo ni lazima apitie matanuri ya moto ili aweze kukomaa,” amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live