Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally amlipua Gamondi, hakuna kocha bora wa aina hii..!

Gamondii X Ahmed Ally Ahmed Ally amlipua Gamondi, hakuna kocha bora wa aina hii..!

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nitashangaa kumuona uyu Mwalimu kwenye tuzo ya Makocha bora msimu huu

Haijalishi ame-achieve nini lakini hastahili chochote kwa utovu wake wa nidhamu uliopitiliza

How come Mwalimu Mkuu unakua na tabia za hivyo?? Ina maana asingezuiliwa angepigana??

Vitendo hivi vinachafua mpira wetu na inaonekana ligi ya wahuni, wasio na ustaaarabu

Kama kila asieridhishwa na maamuzi afanye vurugu hii si itakua ligi ya kina Mwakinyo

Halafu hapo bado wapo kwenye mchezo Mwamuzi huyu alishindwa nini kumuonesha kadi nyekundu??

Hii tabia ya Watu wa Nyuma Mwiko kuwafanyia vurugu Waamuzi imeota mizizi sasa tazama Video ya pili na tatu

Video ya pili ni Watu wa Nyuma Mwiko wakitaka kuwapiga Waamuzi wiki iliyopita kwenye mechi ya Ceasiaa Queens na Nyuma Mwiko Princess katika Uwanja wa Samora Iringa

Waamuzi waliokolewa na Polisi na wakatoka Uwanjan chini ya Ulinzi mkali

Hii tabia inapaswa kukomeshwa tena kwa haraka kwanza usalama wa Waamuzi wetu pili kulinda thamani na hadhi ya mpira wetu

Hatuko tayari kuona watu wachache wanachafua taswira ya mpira wetu na hawa nyuma mwiko lazima wakumbushwe kuwa hawapo juu ya sheria

Chanzo: www.tanzaniaweb.live