Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally alivaa sakata la Kibu Denis

KIBU DENISS Kibu Denis

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: dar24.com

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amejitokeza hadharani na kumkingia kifua Kiungo Mshambuliaji wa Klabu hiyo Kibu Denis.

Kiungo huyo amekuwa na wakati mgumu msimu huu, huku akionyesha kushindwa kuwajibika kwa kuifungia Simba SC mabao muhimu licha ya nafasi anazopata kila anapopewa nafasi na Kaimu Kocha Mkuu Juma Ramadhan Mgunda.

Ahmed Ally amechukua jukumu hilo, kwa kuandika ujumbe mzito kwenye kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kuhusu Kibu, ambaye alisajiliwa Klabuni hapo mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Mbeya City FC.

hmed Ally ameandika: Kila mmoja hupitia nyakati ngumu kazini.

Kibu Denis anapitia nyakati hizo, jukumu letu ni kusimama nae na kumtia moyo ili isimuathiri, Kwenye football ukipatia utapatia tena, na ukikosea unaweza kukosea tena ni jukumu letu kumpa support ili asikosee tena.

Hatupaswi kumpa presha tunapaswa kumpa imani kwamba anaweza kufanya makubwa kama alivyofanya msimu uliopita

Chanzo: dar24.com