Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally afunguka madai ya kumuacha Kagere

Ahmed Ally, Msemaji Simba Ahmed Ally afunguka madai ya kumuacha Kagere

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Simba SC, Ahmed Ally amesema straika wao Meddie Kagere bado ana mkataba na Wekundu hao hivyo ataendelea kuwepo.

Ahmed amesema, Kifaru huyo wa Rwanda bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba na ndio maana ameambatana na kikosi kilichoondoka leo nchini kuelekea Misri.

“Kagere bado yupo kwa mwaka Zaidi ndani ya Simba. Hivyo tutakuwa naye kwa msimu unaokuja,” alisema Ahmed.

Simba wameondoka nchini leo Julai 14, 2022 kuelekea Misri ambapo watakaa pre season kwa takriban wiki tatu kisha kurejea nchini kuanza msimu mpya wa 2022-23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live