Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Washambuliaji tulio nao ndo hao hao, hatuna namna!

Jobe X Freddy Jobe na Fredy.

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo hawapaswi kuanza kuwalamikia wachezaji wao kwa sasa wala kutafuta mchawi baada ya kufungwa na Tanzania Prisons, badala yake waungane kwa ajili ya kuisapoti timu yao kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Union.

Ahmed amesema hayo mara baada ya kutua Tanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Wagosi wa Kaya utakaopigwa kesho Jumamosi katika Dimba la Mkwakwani huku Mnyama akiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons kwa kipigo cha bao 2-1.

“Kufungwa na Prisons kusitutote kwenye reli sasa hivi tukaanza kutafuta mchawi. Mashabiki wana haki ya kuumia kwa sababu wanaipenda timu yao na kama unaishabikia unataka furaha sio huzuni.

“Ukisema washambuliaji hawafai, unamtoa wapi mshambuliaji sasa hivi na hakuna dirisha la usajili? Wachezaji waliopo tuwaunge mkono wanataka sapoti yetu ili kufanya vizuri. Tusimame na timu yetu badala ya kugawanyika.

“Mapungufu yote mwalimu ameyaona na kuyafanyia kazi kwa ajili ya kuboresha na kuleta mbadiliko chanya kwenye mchezo ujao.

“Ni wachezaji hawa hawa waliotupa furaha ya ushindi wa bao 6-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy siku chache tu zilizopita, kwa hiyo tukubali kuna siku nzuri na siku mbaya kazini,” amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live