Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Unbeaten yenu ilijaaa mafindofindo

Ahmed Ally 01 1 1140x640 Ahmed Ally

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewaponda wapinzani wao Yanga baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Klabu ya Ihefu FC yenye makazi yake Mbalali Mkoani Mbeya.

“Unbeaten yenu ilijaa magoli mengi ya offside na Penati za gubu la wifi. Hata jana tayari mlishatengeneza unbeaten ya offside, mfungaji wenu alikua kasimama mbele peke yake kama dereva wa treni.

"Waamuzi zaidi ya wanne wamefungiwa wakiwasaidia kutengeneza unbeaten na mwingine mmoja ameshtakiwa kamati ya waamuzi tunasubiri hukumu. Sisi tunaheshimu ubora wa wapinzani lakini hatuheshimu unbeaten ya mchongo kama yenu.

"Nyie kuendelea kuwa unbeaten ilikua ni kuutukanisha mpira kwa sababu hamna hiyo quality. Niko palee nakula mihogo Kama una makasiriko nawe agiza mihogo na bofya link hii katazame timu yenye quality Bora mnyama Simba SC," amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live