Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Tutapambana hadi kieleweke

Ahmed Ally 01 1140x640 Ahmed Ally: Tutapambana hadi kieleweke

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: Dar24

Wawakilishi Pekee wa Tanzania kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi Simba SC, wamesisitiza kupambana Kufa na Kupona, watakapocheza ugenini dhidi ya Horoya AC mwishoni mwa juma hili (Jumamosi Februari 11).

Simba SC itakua mgeni wa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa General Lansana Conte mjini Counakry, saa kumi kwa majira ya nchini Guinea.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu hiyo ya Msimbazi Ahmed Ally amesema, mipango mikubwa ya Benchi la Ufundi linaloongozwa na Kocha Roberto Oliveira, ni kuona kikosi chao kinapambana na kupata ushindi ugenini.

Ahmed amesema Kocha huyo amekua akiwasisitiza wachezaji wake kuhakikisha hilo linafanikiwa, na kama mambo yatakuwa magumu basi wanapaswa angalau kupata matokeo ya sare ambayo yatakuwa mazuri kwa upande wao.

“Mpango wetu wa kwanza kule Guinea ni kuhakikisha tunapata ushindi. Kama mambo yatakuwa magumu basi tusifungwe na tusishinde.”

“Kiujumla maandalizi mengine ya mchezo wetu wa kwanza wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Horoya AC yanakwenda vizuri.” amesema Ahmed Ally.

Kuhusu mipango yao watakapofika nchini Guinea, Ahmed amesema tayari Uongozi wa Simba SC umewatanguliza baadhi ya maafisa wake, ambao wanafanya kazi kubwa itakayosaidia kikosi chao kuishi kwa amani na utulivu kwa muda wote watakaoishi mjini Counakry.

“Tumeshatanguliza watu Guinea kwa ajili ya Logistics mbalimbali,” ameongeza Ahmed Ally.

Wakati Simba SC ikitarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa Kundi C Jumamosi (Februari 11), Mabingwa wa Soka nchini Morocco Raja Casablanca wataikaribisha Vipers SC mjini Casablanca kwenye Uwanja wa Mfalme Mohammed V Ijumaa (Februari 10), kuanzia saa mbili usiku kwa majira ya Morocco.

Chanzo: Dar24