Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Tunakwenda kupiga kwenye mshono

Ahmed Ally Press Leo.jpeg Ahmed Ally, Ofisa Habari wa Simba SC

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Simba SC umesema licha ya ukweli kuwa wapinzani wao Young Africans wamebadilika kiuchezaji kulinganisha na msimu uliopita, hilo haliwatishi na halitawazuia kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema hayo alipozungumzia mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wengi wa soka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Ahmed amesema wapinzani wao wanaonekana kuongezeka ubora msimu huu hasa kwenye kasi na kukaba.

“Zinapokwenda kucheza timu zinazoshika nafasi ya kwanza na nyingine ya pili, mechi hiyo haiwezi kuwa nyepesi, lakini pia tuseme ukweli Kocha Gamondi ameibadilisha Young Africans kutoka pale ambapo aliiacha kocha Nasreddine Nabi, kuna kitu amekiongeza, kwa hiyo mechi itakuwa ngumu,” amesema Ahmed.

Hata hivyo amesema pamoja na yote hayo Simba ina kikosi cha wachezaji bora ambao wanaweza kuamua matokeo katika mechi yoyote ile.

“Simba SC tunayo faida ya kwenda kufanya vizuri dhidi yao kwa sababu tuna wachezaji bora zaidi yao, wachezaji wamecheza mechi nyingi kubwa na zenye presha, hatuna shaka hata kidogo, pamoja na uimara wao tutapiga pale pale tulipopiga kwenye mechi ya mwisho ya Ligi kuu tulipokutana msimu uliopita,” amesema Ahmed.

Amesema wachezaji wao pamoja na Kocha Robertino wana uwezo mkubwa wa kuikabili Young Africans na timu yoyote Barani Afrika.

Amesema Robertinho anaendelea na maandalizi yake tangu Jumanne (Oktoba 31), kiufundi na kila kitu kinakwenda vizuri akiwa na wachezaji wake wote.

Chanzo: Dar24