Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amewataka Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kujiamini na kutembea kifua mbele, licha ya timu yao kutolewa kwenye Michuano ya African Football League.
Simba SC imetupwa nje ya michuano hiyo mipya Barani Afrika kwa Kanuni ya bao la Ugenini, kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Mabingwa wa Bara hilo Al Ahly, ambao walilazimisha sare ya 2-2 kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam Ijumaa (Oktoba 20).
Ahmed ametoa ushawishi huo kwa Wanachama na Mashabiki wa Simba SC kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii akiandika maneno ya kishujaa, kabla ya kuanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam.
Ahmed Ally ameandika: Hatuwezi kuacha kujivunia perfomance na progress ya timu yetu.
Tumeonesha kwanini FIFA, AFL na CAF walituamini kutuchagua kushiriki mashindano haya.
Mechi yetu itasalia kuwa ndo mechi bora ya michuano hiii Tumeipa heshima AFL.
Sisi ndo timu pekee ambayo tumeondolewa kwenye mashindano bila kufungwa.
Upo wakati mwingine wa kutimiza malengo yetu na hauko mbali. Muhimu ni kuendeleza mipango.
Wana Lunyasi tutembeee kifua mbele timu tunayo, wachezaji tunao na mipango tunayo ni muda tuu utaamua!!!
Najivunia hii timu????????