Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Tumefungwa lakini timu tunayo

Simba Yanga Mzmzm Simba vs Yanga

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa licha ya kufungwa na watani zao Yanga SC, lakini wana kikosi kizuri ambacho wana uhakika kitafanya vizuri msimu huu.

Ahmed amesema hayo baada ya Simba kufungwa bao 1-0 na Yanga kwenye nusu fainali ya Ngao ya Jamii, mchezo uliopigwa katika Dimba la Mkapa.

"Asante Mungu. Ni matokeo mabaya lakini yenye kutupa maono wapi tunaelekea kwenye ujenzi wa kikosi chetu bora msimu huu.

"Tunakila sababu ya kujivunia maendeleo ya project yetu ya muda mrefu iliyohusisha wachezaji wengi wapya wenye vipaji vikubwa na umri mdogo.

"Wana Simba SC matokeo ya leo yasiwatie unyonge kwani tupo katika njia sahihi sana na punde tutaanza kuogelea kwenye mito ya asali.

"Hii ni tofauti na msimu uliopita tulichukua ngao ya jamii lakini hatukua na timu imara ndio maana tukakosa Makombe yote, Msimu huu tumekosa Ngao lakini tunayo timu imara ya kutupa heshima hapo baadae.

"Muda sio Mrefu tu ,Maji yatajitenga na mafuta, muda si mrefu. Memkwa utawaona Muda si Mrefu ngoja tu Ligi ichanganye. Mimi Timu ninayo.

"Mimi Kwa mara yakwanza tangu Nimeanza kazi Simba sijawahi kuona Mashabiki Wanawashangilia Wachezaji huku Timu imepoteza tena umefungwa na Mpinzani wako Namba Moja alafu watu wanashangilia we huoni kama ni Ubaya Ubwela huo.

"Hii Simba sio ya kawaida, hii Simba itakuja Kufanya balaa kubwa mno, hii Simba ni ya kiwango cha hali ya juu mno," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: