Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Tulieni Wanasimba

Ahmed Ally Semaji La Simba.jpeg Ahmed Ally: Tulieni Wanasimba

Sun, 26 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, timu ya Simba SC, imebanwa mbavu nyumbani kwa kulazimishwa sare ya 1-1 na Asec Mimosa ya Ivory Coast.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewatuliza mashabiki wa timu hiyo akisema kuwa kazi bado haijaisha.

"Tumepata alama moja, si nzuri sana na si mbaya sana, Tuna kazi kubwa ya kufanya katika mechi zijazo kuhakikisha malengo yanatimia.

"Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri, tumepoteza alama tatu katika 18 za hatua ya makundi hivyo tumebakiwa na 15 za kupigania.

"Nyakati ngumu zinatukomaza na kutukumbusha tuboreshe wapi kwenye timu yetu. Poleni sana Wana Lunyasi.

Msimamo

Galaxy - goli 1, pointi 3, nafasi ya 1

Asec Mimosas - goli 1, pointi 1, nafasi ya 2

Simba Sc - goli 1, pointi 1, nafasi ya 3

Wydad goli 0, pointi 0, nafasi ya 4.

Mechi zijazo

Galaxy vs Simba

Asec vs Wydad

Tangu msimu huu umeanza, Simba haijashinda mchezo wowote wa Kimataifa.

Power Dynamo 2-2 Simba SC

Simba SC 1-1 Power Dynamo

Simba SC 2-2 Al Ahly

Al Ahly 1-1 Simba SC

Simba SC 1-1 Asec Mimosac.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live