Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Tulichopoteza Moshi ni Kidogo

Ahmed Ally Simbaaa Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba SC Ahmed Ally

Tue, 12 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuambulia sare katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania katika Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hatimaye Simba wameamua kusahau na kuweka mawazo yao katika mchezo dhidi ya Orlando Pirates Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema Wanasimba kwa sasa ni wakati wao kutambua kile kinachokuja mbele yao.

"Tulichopoteza Moshi ni Kidogo kuliko tunachokwenda kukitafuta siku ya Jumapili dhidi ya Orlando, sina nia ya kudharau Ligi yetu lakini ukweli ni kuwa tunakwenda kucheza mechi kubwa ya heshima"

"Niwaombe Wanasimba tujitokeze kwa wingi Uwanjani, tumepewa ruhusa ya kuingiza Mashabiki 60,000 hivyo tunapaswa kuwaonesha ukubwa wa Simba, tukaujaze Uwanja" amesisitiza Ahmed

Chanzo: www.tanzaniaweb.live