Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Thank you zinaendelea Simba

Ahmed Ally Wiki Ya Thank You Ahmed Ally

Sat, 29 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amewatoa hofu wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kuwa michakato ya usajili inaendelea na wako katika hatua za mwisho kukamilika

Baada ya kutoa Thank You kwa wachezaji watano pamoja na kutangaza usajili wa beki Lameck Lawi, ukimya umetawala Msimbazi jambo lililowapa hofu baadhi ya Wanamsimbazi wenye shauku kubwa ya kutaka kufahamu maboresho ya kikosi

"Usajili unaendelea, mpaka sasa umekamilika kwa asilimia kama 97 hivi, hivyo mashabiki wasione kama tuko kimya, tunakamilisha ujenzi wa nyumba yetu"

"Kuanzia wiki ijayo tutaanza kutangaza wachezaji wote tuliowasajili, itakuwa bandika- bandua bila ya kupumzika"

"Najua shauku ya Wanamsimbazi lakini niwahakikishie tumeleta vyuma kwelikweli. Baadhi ya wachezaji tayari wameshatua kwa ajili ya taratibu za maandalizi ya pre-season," alisema Ahmed

Simba inatarajiwa kuondoka nchini wiki ijayo kuelekea Misri kwa ajili ya pre-season itakayodumu kwa wiki tatu na kikosi kurejeea kwa ajili ya Tamasha la Simba Day litakalofanyika August 03.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live