Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Shirikisho sio kombe la 'loser', ni kombe kubwa

Ahmed Kamwez Ahmed Ally na Ally Kamwe.

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa timu yao wanapaswa kupambana kufa na kupona kuhakikisha wanamaliza katika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya NBC ili msimu ujao waweze kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Ahmed amesema hayo mara baada ya kutua Dar wakitokea Bukoba ambako Simba ilikuwa na mchezo wa Ligi dhidi ya Kagera Sugar, mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 katika Dimba la Kaitaba.

“Sare dhidi ya Kagera Sugar huwezi kusema ni homa inakuja inakata, hayo yalikuwa makosa ya wachezaji wetu, ni suala la kuongeza umakini, mechi zetu zilizobaki hatupaswi kukosea kwa sababu ukidongoka kidogo tu unampa nafasi Azam FC.

“Tunatembea juu ya Kamba nyembamba ambapo chini yake kuna bwawa la mamba, ukiteleza kidogo tu chali umeliwa na mamba, unakosa nafasi ya pili unakwenda kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

“Kombe la Shirikisho sio baya, ni michuano mikubwa ya tatu barani Afrika, ina thamani kubwa mno, achana na maneno ya wapuuzi kwamba ni kombe la looser, kwa hiyo sio mbaya kwenda kushiriki lakini kwa ukubwa wetu sisi Simba SC, tunapaswa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kwa hiyo mechi chache zilizosalia, tunapaswa kuwa makini wa asilimia 100 ili tupate ushindi. Kocha Mgunda anayo kazi ya kuwakumbusha vijana wake, tukifanya makosa kama mechi ya Kagera Sugar maana yake ni inaillah wa inalilah rajiun,” amesema Ahmed.

Azam FC wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 60 na michezo 27 huku Simba akiwa nafasi ya tatu na alama 57 katika michezo 26 waliocheza lakini Azam ana idadi kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Endapo Azam na Simba kila mmoja atashinda michezo yake yote, basi watalingana alama na mshindi wa pili ataamriwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Katika hatua nyingine, Bingwa (mshindi nafasi ya kwanza) ambaye ni Yanga ana nafasi ya moja kwa moja ya kushiriki Klabu Bingwa Afrika pamoja na mshindi wa nafasi ya pili. Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika imefutwa rasmi kuanzia msimu ujao haitakuwepo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live