Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Poleni Mashabiki Simba SC

Mashabiki SImba Mkwakwani 1 Mashabiki wa Simba SC

Thu, 22 Dec 2022 Chanzo: dar24.com

Meneja Habari na Mawasilino Simba SC Ahmed Ally amewapa pole Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo, kufuatia matokeo ya 1-1 dhidi ya Kegara Sugar.

Simba SC ilicheza ugenini jana Jumatano (Desemba 21) majira ya Usiku Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba-Kagera, huku ikitangulia kufungwa bao la mapema na wenyeji wao kupitia kwa Deus Bukenya dakika ya 15, kabla ya Simba SC kusawazisha kwa bao la kichwa lililofungwa na Beki kutoka DR Congo Enock Inonga Baka dakika ya 39 Kipindi cha Kwanza.

Ahmed Ally ametumia Kurasa zake za Mitandao ya kijamii kutoa pole hizo kwa Mashabiki na Wanachama, huku akisisitiza mapambano bado yanaendelea ili kufikia malengo waliojiwekea msimu huu 2022/23.

Ahmed ameandika: Pamoja na juhudi zote ambazo wachezaji wetu wamezifanya na kujitoa kwa nguvu na maarifa yote lakini furaha haijaja upande wetu.

Mpinzani amekua bora na hatimae tumevuna alama moja Si nzuri kwetu kulingana na malengo yetu lakini hatuna budi kuipokea na kusonga mbele bado tuna mechi nyingi.

Poleni sana

Chanzo: dar24.com