Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Pa Omar Jobe anaondoka Simba

Pa Omar Jobe Bado Yupo Sana Msimbazi Pa Omary Jobe.

Thu, 4 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imesema kuwa itasafiri kwenda nchini Misri kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao ‘pre-season’ na washambuliaji wawili tu ambao ni Steven Mukwala (usajili mpya) na Freddy Michael (alikuwepo tangu msimu uliopita).

Hayo yamesemwa na Meneja wa habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally wakati akiulizwa kuhusu washambuliaji watakaokuwepo Simba msimu ujao hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya mashabiki wameonesha kutomtaka Pa Omar Jobe huku wakishinikiza aondoke klabuni hapo kutokana na kutokuonesha uwezo tangu asajiliwe.

“Washambuliaji wa Simba ambao tutaondoka nao kwenda ‘pre-season’ nchini Misri ni wawili, yaani Fred Michael na Steven Mukwala. Fred baada ya kumaliza mapumziko nyumbani kwao Ivory Coast, leo amekuja na amefanya vipimo, yuko tayari kwenda pre-season.

“Huyo mwingine (Jobe) siwezi kuthibitisha hapa kwa sababu bado kuna masuala ya kimkataba. Lakini kwa maslahi ya klabu niwathibitishie mashabiki ambao wamekuwa wakiuliza, washambuliaji tegemeo wa Simba tutakaokuwa nao msimu ujao ni hao wawili, Mukwala na Fred.

“Hawa wanatosha kwa maana ya washambuliaji wa kigeni, lakini kuna mzawa mwingine ataongezeka hapo kwa ajili ya kuja kuongeza nguvu zai,” amesema Ahmed.

Pa Omary Jobe hatakuwa sehemu ya timu hiyo. Kuna jitihada zinafanywa na viongozi wa Simba kuachana na Jobe, hivyo kuna uwezekano asiwepo Simba msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: