Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Nampenda Aucho, simpendi Mayele

Ahmedy Simba B Ahmed Ally: Nampenda Aucho, simpendi Mayele

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema anapenda na kuvutiwa uwanjani na mchezaji wa Yanga, Khalid Aucho raia wa Uganda kutpokana na uchezaji wake.

Aidha, Ahmed amemtamja mshambuliaji wa Yanga, Fiston Kalala Mayele raia wa Congo DR kuwa mchezaji asiyemvutia kutokana na kuwaadhibu katika baadhi ya michezo yao.

Ahmed amefunguka hayo akijibu moja kati ya maswali kutoka kwa watangazaji wa kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM wakati wakitaka kujua ni Mchezaji gani kutoka Yanga sc anayemkubali na yupi pia asiye mkubali.

Mayele tangu ajiunge na Yanga ameshawafunga Simba jumla ya bao tatu ambapo msimu wa 2021/22 alipokuwa akijiunga na Yanga katika mchezo wake wa kwanza aliifunga Simba bao 1 na la la ushindi kuisaidia Yanga kutwaa Ngao ya Jamii.

Haikuishia hapo, katika Ligi Mayele bado hajaifunga Simba lakini wakati wa kuanza kwa msimu wa 2022/23, Mayele aiifunga Simba bao 2 huku Yanga ikitwaa Ngao ya Jamii kwa mara nyingine kwa ushindi wa bao 2-1, mabao yote yakifungwa na Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live