Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Kuna watu bado wanateswa na goli 5 za Yanga

Ahmed Ally: Twendeni Uwanjani Hata Kama Tuna Hasira.jpeg Ahmed Ally: Kuna watu bado wanateswa na goli 5 za Yanga

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema kuna watu bado wanateswa na matokeo ya 5-1 dhidi ya Yanga SC katika mechi ya ligi Kuu ya NBC.

Ahmed amesema kwa kulitambua hilo, atapita kwenye kila tawi ili aweze kuhamasisha watu waende uwanjani kwenye yao ya kwanza ya hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa dhidi ya ASEC Mimosas kesho Novemba 25, 2023 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

"Kuna watu huwa hawasahau mabaya kwa haraka ni mpaka muda fulani upite, kwahiyo kuna mtu kila akiwaza niende uwanjani Jumamosi anakumbuka tulifungwa tano. Hivyo tunafanya kazi kubwa ya kuhamasisha watu na binafsi nimechukua juhudi za kupita tawi kwa tawi walau tukaonane na wale wenyewe wenye Simba yao na kuzungumza nao kuwashawishi kwenda uwanjani" - Ahmed Ally- Msemaji wa Klabu ya Simb

Chanzo: www.tanzaniaweb.live