Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Hatuwezi kurudia makosa Jumapili

AHMED ALLY MAKOSA Ahmed Ally: Hatuwezi kurudia makosa Jumapili

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema kamwe hawawezi kurudia makosa ya kupoteza mchezo wa nyumbani baada ya kushinda mchezo wa ugenini.

Ahmed ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari kuhusu mipango mbalimbali waliyoipanga kuelekea mchezo wao wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Aagosto ya nchini Angola utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

"Kikosi chetu kimerejea rasmi mazoezini baada ya juzi kurejea kutokea Angola. Kilianza mazoezi jana asubuhi kwenye uwanja wetu wa Mo Simba Arena na leo kitaingia kambini."

"Tulishinda lakini bado hatujafuzu, safari hii hatutaki kurudia makosa. Tumeweka nguvu kubwa kuona kwamba mchezo wa Jumapili tunapata matokeo mazuri ili tuingie makundi. Tumemiss kushiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika."

Oktoba 24, 2021, Simba walitolewa na Jwaneng Galaxy katika Uwanja wa Mpaka baada ya kupigwa goli 3-1.

Mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Botswana, Simba walishinda 2-0 hivyo Simba wakaaga mashindano kwa kufungwa magoli mengi zaidi wakiwa nyumbani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live