Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: CAF imetupa masharti maalum

Simba Jezi Mpya.jpeg Ahmed Ally: CAF imetupa masharti maalum

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: dar24.com

Wachezaji na Maafisa wa Benchi la Ufundi la Simba SC wataendelea kuvaa vifaa vya Michezo vyenye nembo ya Mdhamini Mkuu wa klabu hiyo Kampuniya M-bet, wakati wa Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Hatua ya Makundi.

Simba SC ni miongoni mwa Klabu 16 za Barani Afrika zitakazoshiriki Michuano hiyo, itakayoendelea tena mwishoni mwa juma hili katika viwanja tofauti Barani humo, huku vikibanwa na Kanuni za udhamini kutoka CAF kwa kutotumia nembo za udhamini wa Kampuni za Ubashiri.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amesema wamepata ufafanuzi wa kina kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kuhusu kuendelea kumtumia mdhamini wao Kampuni ya M-bet, lakini wamepewa masharti maalum.

Amesema Kikosi na Maafisa wa Benchi la Ufundi la Simba SC watakuwa huru kuvaa vifaa vya Michezo vyenye nembo ya Mdhambini wakati wote isipokuwa siku moja kabla ya mchezo na siku ya mchezo.

“Tukisafiri tutakuwa na M-Bet, siku moja kabla ya mechi na siku ya mechi ndio tutakuwa tunatumia Visit Tanzania kama ilivyo matakwa ya CAF.” amesema Ahmed Ally alipotoa ufafanuzi wakati wa uzinduzi wa Jezi maalum za Klabu hiyo watakazozitumia wakati wa Michezo ya Ligi ya Mabingwa Hatua ya Makundi.

Katika hatua nyingine Ahmed Ally amewataka Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kuwa na subra katika suala la kupata jezi mpya za Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Amesema Jezi hizo zitaanza kuuzwa katika sehemu maalum Februari 15 kwa gharama ya Shilingi Elfu 35, lakini wachezaji wataanza kuzitumia kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Horoya AC, utakaopigwa Jumamosi (Februari 11), mjini Counakry.

“Jezi zitauzwa Tsh. 35,000 kwa jezi moja na zitaanza kuuzwa Februari 15. Wachezaji wataanza kuvaa tukienda kucheza na Horoya AC” amesema Ahmed Ally

Jana Jumanne (Februari 07) Simba SC ilizindua Jezi za nyumbani, ugenini na chaguo la tatu zenye dhima ya kuitangaza nchi ya Tanzania ‘Visit Tanzania’, katika hafla maalum iliyofanyika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es salaam.

Chanzo: dar24.com