Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally: Azam lazima watoe tatu kesho

Simba Ahmed Mashabiki Ahmed Ally.

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa nafasi yao ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao watajihakikishia leo endapo wataifunga Azam FC.

Ahmed amesema hayo kuelekea mchezo huo wa Ligi utakaopigwa leo katika Dimba la Azam Complex Chamazi huku Azam akiwa nafasi ya pili alama 57 na michezo 25 na Simba nafasi ya 3 akiwa na alama 50 na michezo 24.

“Moja kati ya malengo ambayo tunayoyapigania ni kuhakikisha tunapata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao, na kikanuni ili kuweza kupata nafasi hiyo lazima uwe nafasi ya Kwanza au ya pili. Na kimsingi Simba bado tunayo nafasi katika maeneo yote mawili.

“Sisi ligi bado hatujamaliza nafasi tunayo na tarehe 09 tunakwenda kupigania. Ushindi wetu mbele ya Azam Fc inatuwekea matumaini ya kuwa nafasi ya Kwanza na kama ngoma ikiwa ngumu tutangukie nafasi ya pili,” amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live