Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahly wafanya yao Ligi ya Mabingwa Afrika, waichapa Esperance de Tunis

IMG 6954.jpeg Al Ahly wakishangilia Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika

Sun, 26 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Al Ahly imefanikiwa kutwaa tena taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Espérance Sportive de Tunis katika mchezo wa marudiano wa Fanali usiku wa jana Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri.

Bao pekee la Al Ahly amejifunga kiungo Mtogo, Roger Ben Boris Aholou dakika ya nne akijaribu kuokoa. Ikumbukwe mechi ya kwanza timu hizo kutoa sare ya bila mabao Mei 18 Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi Jijini Radès nchini Tunisia.

Kwa kutwaa taji hilo la 12 la Ligi ya Mabingwa, Al Ahly watazawadiwa dola za Kimarekani Milioni 4, wakati Esperance watapata dola Milioni 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live