Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahly kutua Dar leo, nyota watatu hati hati kuikosa Yanga

Ahly Mapipa Ahly kutua Dar leo, nyota watatu hati hati kuikosa Yanga

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari na mawasiliano wa Al Ahly, Gamal Gabr amesema timu hiyo itatua nchini leo na wachezaji 25 huku nyota watatu Taher Mohamed, Antony Modeste na Mahmoud Metwaly wakiwa kwenye hatihati ya kuukosa mchezo dhidi ya Yanga wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hizo zilizopo Kundi D zinakutana katika mchezo huo utakaopigwa saa 1:00 usiku huku Al Ahly ikitoka suluhu katika mechi iliyopita ya Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Smouha na kufikisha pointi 14 nyuma ya vinara Pyramids yenye pointi 16.

Yanga inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kundi hilo kwani baada ya hapo itakwenda Ghana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: