Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aguero sio kubet tu, mwamba anazo

Aguero Rasmi Kun Aguero

Mon, 25 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saa chache kabla ya mchezo wa fainali ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia, mchezaji wa zamani wa Manchester City, Atletico Madrid na Barcelona Sergio Kun Aguero aliweka chapisho kwenye akaunti yake ya Instagram akionyesha kwamba ameibetia Man City ushindi wa zaidi ya mabao matatu, kisha akaweka dau la dola 10,000 ambayo ni zaidi ya Sh22 milioni.

Mambo yakajipa na mchezo ukamalizika kwa Man City kushinda mabao 4-0, Aguero akajishindia kiasi cha Dola 20,700 (zaidi ya Sh51 milioni).

Hii sio mara ya kwanza kwa staa huyu kubeti. Ameonekana mara kadhaa akifanya hivyo kwenye baadhi ya mashindano makubwa na muda mwingine hata kwenye mashindano ya kawaida, hii ikiwa ni njia mojawapo ya kujiingizia kipato, lakini je jamaa anaishi kwa kubeti baada ya kustaafu soka ama ana mishe nyingine? Leo tunakuonyesha jinsi anavyopiga pesa kupitia kubeti na sehemu nyingine.

ANAPIGAJE PESA

Kwa mujibu wa mtandao Celebritywealth anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 80 milioni, hiyo inatokana na mshahara aliokuwa akiupata na madili mengine ya nje ya uwanja.

Kwa mwaka mmoja staa huyu alikuwa na uwezo wa kupata hadi Dola 23.5 milioni kupitia mshahara wake ambao alipokuwa Man City kwa wiki alikuwa akipewa Pauni 230,000 lakini alipoenda Barcelona mshahara huo ulipungua na kufikia Pauni 150,000 kwa wiki.

Mbali ya mshahara Aguero hadi sasa anapata kiasi kisichopungua Dola 5 milioni kwa mwaka kutokana na madili ya nje ya uwanja ambayo amesaini ikiwa pamoja na ubalozi wake na kampuni za Puma, Pepsi na Electronic Arts.

Kupitia kubeti hadi kufikai sasa anaripotiwa kukunja zaidi ya Pauni 1 milioni (Sh3.2 bilioni za Kitanzania).

MSAADA KWA JAMII

Amekuwa akifanya kazi kwa karibu na rafiki yake Lionel Messi kupitia taasisi ya Leo Messi Foundation lakini pia ni mmoja ya wadau wakubwa wa mfuko wa Teenage Cancer Trust. Pia anatambulika kama balozi wa kutetea haki za binadamu.

MAGARI

Hivi karibuni alinunua gari mpya aina ya Ferrari SF90 Stradale yenye thamani ya Pauni 400,000 (Sh1.2 bilioni za Kitanzania) lakini mbali ya hiyo alishakuwa na gari nyingine nne nyumbani ambazo ukijumlisha zote kwa pamoja zinakadiriwa kufikia Pauni 3 milioni. Gari nyingine ni- ERRARI GTC4 LUSSO, LAMBORGHINI AVENTADOR, LUMMA CLR SV RANGE ROVER

NISSAN GT-R

UHUSIANO

Yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mrembo anayefanya kazi ya umodo, Sofia. Wawili hao wameripotiwa kukutana huko Buenos Aires, Argentina na wakaanza uhusiano mwaka 2019.

Kabla ya hapo Aguero alikuwa kwenye ndoa na Giannina Maradona, binti wa gwiji wa soka Diego Maradona, aliyemuoa mwaka 2008 na ndoa ikavunjika mwaka 2012 huku wawili hao wakifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Benjamin Aguero.

MJENGO

Anamiliki nyumba yenye thamani ya Pauni 12 milioni huko Miami nchini Marekani. Nyumba hiyo iliyo pembezoni mwa bahari kama zilivyo nyumba nyingine za wachezaji ina kiwanja cha kuchezea soka na eneo kubwa, ndani yake pia kuna hadi bwawa la kuogelea, aliinunua mwaka jana.

Kule jijini Manchester jamaa alikuwa na mjengo wenye thamani ya Pauni 4 milioni.

BATA

Anapenda starehe na baada ya kuachana na soka amekuwa akijivinjari sana maeneo ya starehe kama huko Dubai, ndio maana akanunua hadi mjengo huko Miami sehemu ambayo inasifika kwa starehe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live