Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aguero kuachana na Soka mazima, Kutangaza maamuzi yake kesho

Sergio Kun Aguero Sergio Kun Aguero

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Argentina na Barcelona, Sergio Kun Aguero atatangaza mustakabali wake katika soka siku ya kesho Disemba 15, katika Mkutano na Waandishi wa Habari.

Katika Mkutano huo Aguero ataambatana na Rais wa Klabu ya Barcelona, Laporta pamoja na wachezaji wenzake wa Kikosi cha Barcelona.

Taarifa za awali zinadai kuwa Aguero anatarajiwa kutangaza kustaafu Soka la ushindani kutokana na matatizo ya moyo yanayomkabili.

Aguero amejiunga na Barcelona dirisha la usajili lililopita baada ya kumaliza mkataba wake na Man City.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live