Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aguero amkingia kifua Lionel Messi, Kichapo kinamuhusu (+Video)

Video Archive
Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa zamani wa Argentina Sergio Kun Aguero ameibuka na kumkingia kifua nyota wa Taifa hilo Lionel Messi kufuatia madai ya kuidhihaki nchi ya Mexico kwa kuikanyaga Jezi ya timu yao ya Taifa baada ya mchezo wa Kombe la Dunia.

Madai hayo yameibuliwa na bondia maarufu wa Mexico Canelo Alvarez ambaye kupitia twitter, ametoa vitisho vikali kwa Lionel Messi kwa kumwambia aombe sana asimkamate. Sergio Aguero kupitia twitter ameibuka na kumwambia Canelo Alvarez kwamba

“Bwana Canelo, usiangalie kwenye matatizo tu, kiukweli hufahamu chochote kuhusu mpira na kinachokuwa kinatokea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Jezi siku zote huwa zinakuwa chini baada ya mechi kumalizika kutokana na Jasho. Na kama ukitazama vizuri, Messi alionekana akiigusa Jezi hiyo kwa bahati mbaya wakati anavua kiatu chake.” ameandika Aguero.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live