Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aguero: Messi anarudi Barcelona

TALKSPORT MESSI AGUERO Aguero: Messi anarudi Barcelona

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa zamani wa Argentina, Sergio Aguero anaamini kuna asilimia 50 kwa swahiba yake, Lionel Messi kurudi kucheza Barcelona kabla ya kutundika daruga.

Messi, 35, aliachana na Barca mwaka 2021 baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka 21 na kwenda kujiunga na Paris Saint-Germain kwa mkataba wa miaka miwili. Mwishoni mwa msimu huu mkataba wake utakwisha huko Parc des Princes na atakuwa mchezaji huru na bado haijafahamika kama atabaki kwenye kikosi cha PSG.

Na Aguero anaamini rafiki yake huyo atarudi kumalizia mpira wake Nou Camp, aliposema: “Nafikiri Leo Messi atakwenda kustaafu Barca. Barcelona ni nyumbani kwake na anapaswa kwenda kumalizia maisha yake ya soka pale. Hisia zangu zinaniambia kuna asilimia 50 ya uwezekano wa kurudi Nou Camp.”

Rais wa Barcelona, Joan Laporta kwa zaidi ya mara moja amekuwa akizungumzia uwezekano wa klabu hiyo kumrudisha supastaa Messi kwenye kikosi chao. Hata hivyo, ishu yote hiyo itawezekana kama Barca watakuwa vizuri kiuchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live