Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aggrey Morris azidi kuimarika Azam FC

Aggrey  Morris Skills Aggrey Morris azidi kuimarika Azam FC

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Azam FC, Aggrey Morris ambaye kwa sasa anakaa benchi kama kocha msaidizi amesema yapo mengi aliyojifunza kutokana na kuwaangalia wengine wanapocheza uwanjani.

Morris aliyasema hayo wakati anazungumzia mechi ya timu hiyo dhidi ya Simba iliyomalizika kwa sare ya 1-1 na kufafanua ni rahisi kugundua makosa akiwa nje, tofauti na anapocheza kutokana na kuwa na presha kubwa uwanjani.

"Mfano timu inayoongoza ndio inayokuwa na presha zaidi ya kulinda bao na kuongeza lingine, wakati huo huo mpinzani akiwa vizuri anakuwa anashambulia muda wote ili kusawazisha, hivyo ni jukumu la kila mchezaji kujua mechi ni dakika 90 ndio inayoweza kutoa majibu ya kufanikiwa au la," alisema Morris ambaye ni kocha mchezaji wa timu hiyo aliyoitumikia kwa muda mrefu.

"Simba ilifanya safu yetu ya ulinzi iwe na presha kubwa, kwani ilikuwa inahitaji ushindi ama sare, ndio maana nasema timu inayoongoza inakuwa na mzigo wa kujilinda na kusaka bao lingine ili kujiweka sehemu ya usalama zaidi," aliongeza Morris na kusisitiza anapokuwa benchi, anakuwa anajifunza vitu vingi ambavyo si rahisi mchezaji anayekuwa ndani ya uwanja kuvigundua kwa haraka, kwani anakuwa yupo kwenye presha kubwa ya kuipambani timu kushinda.

"Ndio maana sishangai mashabiki wanapokuwa wanakosoa ama kulalamika, kwani hata wao ni ngumu kujua presha ya ndani ya uwanja, hilo nimeliona sana baada ya kuanza kukaa kwenye benchi," alisema beki huyo wa kati wa zamani wa Taifa Stars na kuongeza; "Kikubwa ninachoweza kusisitiza mchezaji asikubali kuridhika hadi atakapokisikia kipenga cha mwamuzi cha kumaliza mchezo ndipo aone timu yake ipo salama."

Chanzo: Mwanaspoti