Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afya ya Pele yatetereka kwa mara nyingine

Edson Pele Pele

Thu, 22 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshindi mara tatu wa Kombe la Dunia Pele hali yake inaendelea kutetereka akiwa hospitalini akisumbuliwa na maradhi ya kansa.

Pele, 82, ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu katika Hospital ya Israelita Albert Einstein nchini Brazil inaelezwa na binti yake kuwa baba yake atasherehekea Christmas akiwa hospitalini ikiwa ni wiki ya tatu sasa.

“Maradhi yanayomsumbua yamefikia pabaya hivyo anahitaji uangalizi wa karibu”, ameandika Kely Nascimento binti wa Pele kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Pele anashikilia rekodi ya ufungaji bora akiwa na bao 77 ndani ya Brazil kwenye mechi 92 huku akishikilia rekodi ya kushinda taji la Kombe la Dunia mara tatu 1958, 1962 na 1970.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live