Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afutiwa Mkataba kisa visa vya Israel

Anwar Anwar Anwar El Ghazi

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Mainz ya Bundesliga imesitisha mkataba wa winga Anwar El Ghazi raia wa Uholanzi kufuatia machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii kuhusu vita vya Israel na Hamas.

Haya yanajiri ikiwa ni siku mbili baada ya El Ghazi kupinga taarifa ya Mainz juu ya kusimamishwa kwake hapo awali akidai kuwa hajutii kuwaunga mkono Wapalestina.

Mnamo Oktoba 17, 2023, Mainz ilimsimamisha El Ghazi kwa madai ya kuchapisha na kisha kufuta ujumbe kuhusu vita hivyo hatua ambayo klabu hiyo iliona haikubaliki.

Siku ya Jumatatu klabu hiyo ilimuondolea adhabu ya kusimamishwa na kudai kuwa imempa onyo. Katika taarifa yake Mainz ilibainisha kuwa El Ghazi anajuta kuchapisha chapisho hilo na pia alijutia kuhusu athari za chapisho hilo na kuongeza kuwa mchezaji huyo alisema kwamba hakuhoji haki ya kuwepo kwa Israel.

Hata hivyo katika chapisho lingine kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumatano El Ghazi alidokeza kuwa klabu hiyo imetoa taarifa hiyo bila idhini yake kubainisha kuwa:-

"Sijutii wala sihisi kujutia nafasi yangu, sijitengi na nilichosema na ninasimama, leo na daima hadi pumzi yangu ya mwisho, kwa ajili ya ubinadamu na wanaokandamizwa." Aliandika El Ghazi.

Sasa Mainz imeamua kusitisha mkataba na nyota huyo lakini Mholanzi huyo amekuja na chapisho lifuatalo baada ya kusitishiwa mkataba wake.

“Simamia kwenye ukweli, hata kama itakulazimu kusimama peke yako. Upotevu wa riziki yangu si kitu ukilinganisha na mateso wanayofanyiwa watu wasio na hatia na walio hatarini huko Gaza.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live