Mchezaji wa Monaco Mohamed Camara raia wa Mali amefungiwa mechi nne za Ligi Kuu Ufaransa (LFP) baada ya kuziba nembo ya kusapoti ‘Mapenzi ya Jinsi Moja’ (LGBTQ+) kwenye Jezi yake kwenye mechi ya Ligue 1.
Mchezaji wa Monaco Mohamed Camara raia wa Mali amefungiwa mechi nne za Ligi Kuu Ufaransa (LFP) baada ya kuziba nembo ya kusapoti ‘Mapenzi ya Jinsi Moja’ (LGBTQ+) kwenye Jezi yake kwenye mechi ya Ligue 1. Mapema wiki iliyopita, Waziri michezo Amelie Oudea-Castera alisisitiza mchezaji huyo kupewa adhabu nzito kutokana na kukiuka maagizo hayo kwa kuziba nembo inayohamasisha mambo hayo kwenye mchezo dhidi ya Nantes ambapo walishinda 4-0 huku yeye akitupia goli moja kwa mkwaju wa penalti.