Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afungiwa Miezi 6 kwa kumpiga mwamuzi

Beki Afungiwa Mchezaji wa timu ya Police FC Rwanda beki Ndizeye Samuel

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa timu ya Police FC Rwanda beki Ndizeye Samuel amesimamishwa kujihusisha na soka kwa muda wa miezi sita baada ya kumpiga kichwa mwamuzi.

Katika wiki ya 16 ya Ligi Kuu Rwanda, timu ya Police FC ambayo ndiyo ilikuwa mwenyeji wa mchezo iliweza kupoteza kwa kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Sunrise FC.

Ndizeye Samuel mchezaji wa kimataifa wa Burundi alimpiga mwamuzi Nsabimana Patrick ambaye alikuwa kibendera namba mbili baada ya kutoridhishwa na maamuzi yake.

Tukio hilo ni baada ya kukataa bao ambalo lilikuwa limefungwa na Nahoha wa Police FC Nshuti Dominique Savio ikidaiwa kuwa alikuwa ameotea.

Hata hivyo Police FC imekataa rufaa kuhusiana na adhabu aliyopewa mchezaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live