Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika itatinga fainali ya kombe la dunia 2026-rais wa Caf Motsepe

Afrika Itatinga Fainali Ya Kombe La Dunia 2026 Rais Wa Caf Motsepe Afrika itatinga fainali ya kombe la dunia 2026-rais wa Caf Motsepe

Thu, 22 Dec 2022 Chanzo: bbc

Bara la Afrika litatinga fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2026, rais wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) Patrice Motsepe alisema Jumatano alipokuwa akitafakari kampeni ya bara hilo yenye mafanikio nchini Qatar.

Afrika Kusini inaamini kwamba hatua ya awali ya Morocco kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar imeweka msingi kuhusu imani na matarajio kuelekea fainali zijazo.

"Nina imani kwamba katika Kombe lijalo la Dunia, bara la Afrika litaenda mbali zaidi," mzee huyo wa miaka 60 alisema.

"Mafanikio ya kihistoria ya Morocco yametufanya sisi sote barani Afrika kuwa na fahari ya kipekee.

Mustakabali wa soka la Afrika ni mzuri sana. "Ukiangalia vipaji katika bara, kuna mataifa 10-15 barani Afrika kwa sasa ambayo yanaweza kushindana kwa kiwango cha juu zaidi ulimwenguni na kushinda."

Ni madai ya kijasiri ikizingatiwa kuwa Morocco, iliyochochewa na uungwaji mkono wa ajabu wa 'nyumbani' kutokana na ukaribu wa Qatar na Afrika Kaskazini, ndiyo timu pekee iliyowahi kutinga nusu fainali, kati ya ziara 54 za Afrika kwenye michuano hiyo.

Hata hivyo, baada ya Kombe la Dunia lililofanikiwa zaidi barani Afrika, Motsepe pia alikumbuka kuwa bara hilo liliwahi kushinda Olimpiki - kupitia Nigeria (1996) na Cameroon (2000).

Chanzo: bbc