Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika Kusini wapewa mapumziko baada ya kushinda kombe la dunia

Afrika Kusini Wapewa Mapumziko Baada Ya Kushinda Kombe La Dunia Afrika Kusini wapewa mapumziko baada ya kushinda kombe la dunia

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza siku ya mapumziko baada ya nchi hiyo kushinda Kombe la Dunia la Raga la 2023 mjini Paris siku ya Jumamosi.

Springboks walishinda kwa mara ya nne Kombe la Dunia la Raga wikendi, wakiwashinda New Zealand kwa pointi moja, 12-11.

Rais alisema amefanya uamuzi huo "katika kusherehekea mafanikio makubwa ya Springboks" katika hotuba ya kitaifa Jumatatu.

Itafanyika tarehe 15 Disemba.

Bw Ramaphosa alisema serikali ilitaka siku hiyo iwe "siku ya matumaini, siku ya sherehe na umoja. Wanamichezo wetu na wametuonyesha kile kinachowezekana".

Ushindi huo umepongezwa na rais huyo kuwa ni ishara ya matumaini, huku nchi hiyo ikikabiliwa na kiwango cha juu zaidi cha ukosefu wa ajira duniani kwa asilimia 42, pamoja na matatizo mengine ya kiuchumi yakiwemo viwango vya juu vya umaskini na kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Kufuatia ushindi wa timu hiyo katika Kombe la Dunia huko Stade de France, Bw Ramaphosa alisema anataka umoja wa timu hiyo uwe sifa kuu ya jamii.

"Tunahitaji zaidi ya haya, na sio tu katika uwanja wa mafanikio ya michezo," alisema, akionyesha kwamba idadi ya wachezaji weusi kwenye kikosi imepanda kutoka mmoja mwaka 1995 hadi karibu nusu ya wachezaji wa Afrika Kusini katika fainali ya 2023. .

Chanzo: Bbc