Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga S, Ali Kamwe amesema, anazo taarifa kutoka Afrika Kusini jinsi wanavyowzaungumza Yanga SC.
"Juzi niligundua kwamba, watu wanaonunua tiketi za VIP wengi wanatoka nje ya nchi, kwa sababu tumepokea emails na simu nyingi kutoka Kenya, Uganda, Malawi na Zambia wakihitaji tiketi.
"Tumepata picha kwamba, ukubwa wa hii mechi sio tu hapa Tanzania! Hata mashabiki wengine wa nchi jirani wanataka kuishuhudia mechi yetu.
"Mechi yetu na Mamelodi inazungumzwa Afrika nzima kwa sababu kwa sasa Mamelodi ndio timu yenye mvuto Afrika halafu Yanga ndio surprise package.
Hata kwenye mijadala ya watu wa Afrika Kusini wanasema hawapaswi kuichukulia poa Yanga kutokana na kile ilichofanya msimu uliopita kwenye Kombe la Shirikisho kwa sababu wanaweza kukifanya kwenye Ligi ya Mabingwa."