Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afisa wa Mamelodi yamkuta Sudan, arudishwa Afrika ya Kusini

Mamelodi Officer Arudishwa Khaled Ali

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Mamelodi Sundowns imemrejesha nchini Afrika Kusini mfanyakazi wake Khaled Ali aliekuwa nchini Sudan kwa ajili ya uchunguzi kufuatia kauli yake aliyoitoa kupitia mtandao wa Twitter.

Khaled Ali ambaye ni mratibu wa Safari na Mahusiano alinukuliwa akisema kwamba atajitolea kuwapa mashabiki wa Al Ahly data ya uchambuzi kuhusu Al Hilal kabla ya mechi yao ya mwisho.

Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa Al Ahly Marcel Koller amesema anatumai Mamelodi Sundowns watakuwa waadilifu na wenye maadili katika mechi zao mbili za Makundi zilizosalia huku akisema kila mtu anajua uwezo wa Mamelodi Sundowns.

Mamelodi Sundowns tayari imeshafuzu hatua ya makundi huku Al Ahly wakiombea Al Hilal afungwe mchezo ujao wa nyumbani dhidi ya Mamelodi Sundowns halafu wao washinde dhidi ya Coton Sports ili mchezo wa mwisho ambao utawakutanisha Ahly na Al Hilal mshindi asonge mbele.

Bahati mbaya wakati Ahly akiomba Mamelodi Sundowns ashinde Sudan,yeye alishindwa kushinda na mchezo wa kwanza wa Mamelodi Sundowns dhidi ya Al Hilal tena Mamelodi akiwa nyumbani uliisha kwa Mamelodi kushinda ushindi mwembamba wa bao moja.

Al Hilal wanafahamu kuwa wanaweza wasipate alama ugenini kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Al Ahly hivyo wachezaji, benchi la Ufundi na hata mashabiki wanaamini mchezo ujao dhidi ya Mamelodi Sundowns ni kama fainali kwao na kibaya zaidi kwa Al Ahly Mamelodi Sundowns sio mchezo muhimu kwake!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live