Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afcon 2023: Afrika Kusini yaishtumu Nigeria kwa kuwaonya raia wake nchini humo

Afcon 2023: Afrika Kusini Yaishtumu Nigeria Kwa Kuwaonya Raia Wake Nchini Humo Afcon 2023: Afrika Kusini yaishtumu Nigeria kwa kuwaonya raia wake nchini humo

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Mzozo wa kidiplomasia umezuka kati ya Nigeria na Afrika Kusini kabla ya mechi ya nusu fainali ya timu hizo mbili kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika siku ya Jumatano.

Kamishna Mkuu wa Nigeria nchini Afrika Kusini amewaonya mashabiki wa soka wa Nigeria kujiepusha na sherehe za kelele ikiwa timu yao itashinda.Onyo hilo lilikusudiwa kuzuia uchochezi wa mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni kutoka kwa wafuasi wa Afrika Kusini waliokatishwa tamaa.

Lakini Afrika Kusini inasema kuwa hii imezua tu "wasiwasi ".Kumekuwa na ushindani wa muda mrefu kati ya wababe hao wawili wa soka - Super Eagles na Bafana Bafana.

Lakini katika taarifa yake ya Jumanne, Idara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini (Dirco) ilisema "hakuna historia ya uhuni wa soka miongoni mwa Waafrika Kusini" katika mechi dhidi ya Nigeria.

"Tuna imani kwamba taifa linalopenda michezo la Afrika Kusini halina tishio lolote kwa raia wa Nigeria, na hatukubaliani na wasiwasi ulioonyeshwa na Tume Kuu," Dirco aliongeza."

Ushauri huo unasikitisha kwa sababu unaonekana kuleta wasiwasi na mvutano usiokuwa wa lazima kati ya raia wa Afrika Kusini na Wanigeria wanaoishi au kutembelea Afrika Kusini."

Nigeria bado haijajibu kauli ya maafisa wa Afrika Kusini.

Katika miaka ya hivi karibuni, Afrika Kusini imeshuhudia wimbi la mashambulizi ya chuki dhidi ya Waafrika ambao wamehamia huko kutoka sehemu nyingine katika bara, mara nyingi kwa ajili ya fursa bora za kiuchumi.

Katika taarifa yake mapema Jumanne, huduma ya kidiplomasia ya Nigeria ilisema ilikuwa ikitoa onyo hilo kwa sababu imeona ushahidi wa "vitisho vilivyofichwa" na Waafrika Kusini mtandaoni.

Iliwashauri Wanigeria wanaoishi Afrika Kusini "kuwa makini na matamshi yao, wawe makini na wapi wanachagua kutazama mechi hasa katika maeneo ya umma, na wajizuie kushiriki katika sherehe za sauti, ghasia au za uchochezi iwapo Super Eagles watashinda".

Mechi hiyo itachezwa mwendo wa saa mbili ysiku saa za Afrika Mashariki siku ya Jumatano katika jiji la Bouaké nchini Ivory Coast.

Nusu fainali nyingine ni kati ya wenyeji Ivory Coast na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Chanzo: Bbc