Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afadhali yetu tuna Wallace Karia

Wallace Karia Rais wa TFF, Wallace Karia

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Hugo Broos, amelalamikia kukosa ushirikiano kutoka bodi ya ligi (PSL) pamoja na vilabu vya ligi kuu nchini humo.

“Nilijaribu mara nne kuwa na kikao na makocha wote wa timu za ligi kuu, lakini nilisusiwa na bodi ya ligi,” alisema kocha huyo akiongea na vyombo vya habari vya Ubelgiji kabla ya mchezo wao wa kwanza wa AFCON dhidi ya Mali, juzi Jumanne.

“Barua yangu ya maombi ya kikao na makocha hata haikupelekwa na bodi ya ligi kwa vilabu husika. Unaweza mwenyewe ukaona hapo kwamba hakuna maelewano kati ya bodi ya ligi na chama cha soka cha kitaifa.

Matokeo yake nilikataliwa mara tatu kuingia uwanja wa Orlando Pirates kuangalia mechi. Unaweza kupata picha gani hapo?"

Broos hakuishia hapo, alienda mbali na kumtaja kocha wa Mamelodi Sundowns, Rulan Mokwena, kama mtu mjivuni anayeogopwa na kila mtu nchini humo.

“Kocha wa Sundowns, ndiyo Mourinho wao wenyewe. Basi anajifanya Mungu na kila mtu anamsikiliza yeye anachokisema.

Aliwahi kunifokea eti kwa sababu wachezaji wake wawili walirudi kutoka timu ya taifa wakiwa majeruhi.”

KONGOLE KARIA

Kauli hizi za kocha huyo mwenye miaka 71 ndizo zinazonifanya nimpe maua yake Rais wa mpira wetu, Wallace Karia.

Akiwa kama muasisi wa Bodi ya Ligi ambayo ilianza kama kamati ya ligi huku yeye akiwa mwenyekiti, Karia ametengeneza utulivu mkubwa sana baina ya taasisi hizi mbili zinazoendesha mpira wetu.

Timu za taifa husimamiwa na vyama vya soka vya kitaifa, lakini vyama hivyo havina wachezaji zaidi ya kuwategemea wale wa vilabu vilivyo chini ya bodi ya ligi.

Kama hakuna maelewano baina ya chama cha soka cha kitaifa na bodi ya ligi, matatizo kama ya Afrika Kusini lazıma yatatokea.

Hata Tanzania wakati fulani kabla ya Karia kuwa Rais, hali kama hiyo ilianza kujitokeza baada ya bodi ya ligi kuwa na mahusiano mabaya na TFF.

Moja ya hatua kabambe ambazo Karia alizichukua kuhakikisha taasisi hizi mbili zinakuwa na husiano bora ni kumfanya mwenyekiti wa bodi ya ligi kuwa makamu wa pili wa Rais wa TFF.

Haya yalikuwa maamuzi sahihi ya Karia katika kujenga mahusiano tambarare na kuufanya mpira wetu utembee kwenye barabara ya lami.

Hongera sana Karia!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live