Soka lililopigwa na Kiungo kutoka nchini Nigeria, Etop Udoh limewagawa mabosi wa Klabu hiyo wakitaka achukuliwe katika dirisha hili dogo na wengine wakitaka rungu la maamuzi aachiwe Kocha Pablo Franco.
Kiungo huyo ambae amewahi kukipiga katika nchi za Tunisia, Armenia na Saudi Arabia, ni kati ya wachezaji watatu waliojiunga na mabingwa wa Tanzania kwa ajili ya kufanyiwa majaribio kabla ya kusajiliwa.
Wengine ni Sharraf Shiboub na Cheick Moukoro kutokea nchini Ivory Coast na wanacheza jaqpo kwa uchache katika michuano ya Mapinduzi Cup inayoendelea visiwani Zanzibar.
Taarifa zinadai kuwa Kocha amevutiwa zaidi na Udoh ambae kwa dakika chache alizocheza katika mechi iliyoisha kwa sare dhidi ya Mlandege.
Taarifa za uhakika zinadai kuwa mmoja wa watu wazito ndani ya Simba alievutiwa na Kiungo huyo ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah "Try Again", mjumbe wa bodi Mlamu Nghambi na Crescentius Magori lakini wamebaki kimya wakimpa mwalimu nafasi ya kuamua.
Kiungo huyo alipotakiwa atolee ufafanuzi kile anachokionesha ndani ya Simba alisema;
"Naamini nitafanya vyema,nakiamini kiwango changu, kama itashindikana kubaki hapa sio kwa sababu ya kiwango changu labda ni kitu kingine".