Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adolf: Kwa Azam hii, nyie subirini tu!

Adolf Mtasingwa Adolf Mtasingwa

Sun, 21 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo mkabaji wa Azam FC aliyekuwa akihusishwa na Yanga, Adolf Mtasingwa amekiri kwa namna timu hiyo ilivyofanya usajili wa kiwango cha juu anaona itasumbua katika michuano itakayoshiriki tofauti na misimu mingine ambayo ilikuwa inachemsha kizembe.

Adolf alisema usajili uliofanywa na timu hiyo ni wazi wana dhamira ya kufanya vizuri ndani na anga la kimataifa huku akikiri, wakiwa kambini huko Morocco wanaifuatilia kwa ukaribu APR ya Rwanda watakayoumana nayo katika mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

APR ipo nchini ikishiriki michuano ya Kombe la Kagame 2024 na leo itacheza mchezo wa fainali dhidi ya Red Arrows ya Zambia ikisaka taji la nne la michuano hiyo iliyoasisiwa mwaka 1967 na kikosi cha Azam chenyewe kipo Morocco lakini kimekuwa kikiifuatilia michuano hiyo ili kuwasoma Wanyarwanda hao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Adolf alisema wanaendelea na maandalizi huku akikiri kuwa mastaa wengi walioongezwa dirisha hili la usajili wanaonyesha uwezo mkubwa anaamini kama watafanya hivyo hadi kwenye michuano ya ushindani timu yao itafanya poa kimataifa na ndani.

“Msimu ulioisha tumefanikiwa kumaliza katika nafasi ya pili na kupata nafasi ya uwakilishi Ligi ya Mabingwa sasa kuna mastaa wengine wapya ni balaa, naamini watakuwa chachu ya Azam FC kuweza kuwa bora na kufikia malengo ya kucheza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa na kutwaa taji la ligi,” alisema Adolf aliyebakisha miezi 6 Azam.

Chanzo: Mwanaspoti