Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adebayor: Victor Osimhen akacheze EPL

Victor Osimhen.jpeg Adebayor: Victor Osimhen akacheze EPL

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Arsenal na Man City, Emmanuel Adebayor amesema anaamini Victor Osimhen atafanya vizuri katika Ligi Kuu ya England (EPL) kama atajiunga nayo.

Osimhen amekuwa akitamaniwa na timu nyingi zinazoshiriki EPL kutokana na uwezo wa kufumania nyavu, ambao amekuwa akiuonyesha katika kikosi cha SSC Napoli anakocheza hivi sasa.

Klabu za Chelsea, Man United na Arsenal zimekuwa zikimtaka mshambullaji huyo na Adebayor anaamini kama nyota huyo wa Nigeria atajiunga na mojawapo ya timu hizo hatakamatika.

“Ana haiba sahihi na ari ya kupiga hatua kule (England). Ninaombea ahamie katika Ligi Kuu ya England na aonyeshe kile kilicho ndani ya uwezo wake,” amesema Adebayor.

Osimhen mwenye umri wa miaka 25, msimu uliopita ndiye alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Italia kutokana na mabao yake 26 aliyofunga SSC Napoli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live