Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adebayor, Moses Phiri waiteka Simba

SIMBA PHIRI ADEBAYOR Adebayor NA Moses Phiri

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HABARI njema kwa mashabiki wa Simba kwa sasa ni taarifa za rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji, kufungukia mipango ya usajili wa wachezaji wawili Moses Phiri na Adebayor kutua ndani ya timu hiyo katika dirisha kubwa la usajili huku wadau wakubwa wa Simba wakifurahishwa na taarifa hizo njema.

Moses Phiri, mwenye uraia wa Zambia, kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Zanaco, amekuwa akiwindwa pia na watani wa Simba, Klabu ya Yanga huku Victorien Adebayor mwenye uraia wa Niger, anayekipiga katika Klabu ya US Gendarmarie pia akiwa katika mazungumzo na uongozi wa Simba.

Akizungumza, kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Malota Soma ‘Ball Jagler’ yeye alisema kuwa utakuwa ni usajili mzuri kwa Simba kutokana na aina ya wachezaji hao kuwa bora na watawafaa katika michuano ya kimataifa kutokana na uwezo wao na mahitaji ya klabu hiyo.

“Ni wachezaji wazuri sana, Moses Phiri ukimtazama anaweza kucheza nafasi zote za mbele kuanzia winga ya kulia na kushoto lakini kama namba kumi au mshambuliaji wa kati, kote huko anafaa kucheza na anafanya vizuri sana, hivyo kama akisajiliwa basi ataiongezea kitu kikubwa sana Simba.

“Kwa upande wa Adebayor pia ni mchezaji mzuri, yeye nimemtazama katika mchezo mmoja pekee dhidi ya Simba ambapo alisumbua sana, kama ndio yupo hivyo siku zote basi atakuwa msaada mzuri kwa Simba maana inahitaji wachezaji wenye ubora mkubwa ili iweze kufanya vizuri katika michuno ya kimataifa,” alisema mchezaji huyo mstaafu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live