Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adam Salamba asaini JS Soura

Adam Salamaba (600 X 604) Mtanzania Adam Salamba (aliyevaa kofia)

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Adam Paul Salamba amejiunga na klabu ya JS Saoura ya Algeria kutoka Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi.

Salamba ametambulishwa wikiendi iliyopita na tayari ameanza kazi katika klabu hiyo mpya yenye kumbukumbu nzuri za huduma ya Mtanzania mwingine, Thomas Emmanuel Ulimwengu.

Salamba aliibukia Stand United mwaka 2016 kabla ya kwenda Lipuli FC mwaka 2017, ambako alifanya vyema Ligi kuu na kusajiliwa na Simba SC 2018.

Kutokana na kukosa nafasi akajiunga na Al-Jahra SC ya Kuwait 2019, kabla ya kujiunga na Namungo FC 2020.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live