Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ada kusomea taaluma ya " Video Analyst" usipime

Video Analyst,, Ada kusomea taaluma ya " Video Analyst" usipime

Fri, 19 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtathimini mchezo (Video Analyst), Faraji Muya ‘Enzo’, amesema kozi ya taaluma hiyo, haipatikani nchini kwa sasa na wanaohitaji wanasoma kwa njia ya mtandao (online) kutoka Bara la Ulaya.

Enzo aliyesoma ngazi ya cheti (Certificate), alifafanua pia kozi hiyo ada yake imechangamka na inabadilika kwa kadri muda unavyokwenda.

“Kulingana na muda unaosoma, zipo kuanzia miezi mitano, saba na kuendelea, ada inaanzia Sh1 milioni, kulingana na muda ambao unasoma, zingine ni hadi Sh4 milioni,” alisema Enzo na kuongeza;

“Nilisoma kozi hiyo mwaka jana (2023), kiukweli ni nzuri, bado nina mpango wa kusoma ngazi ya juu zaidi, najipanga.”

Ukiachana na taaluma yake ya utathimini mchezo ni kocha wa fitinesi ambayo ana levo ya cheti, alisomea mkoani Tanga, iliyoendeshwa chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

“Katika soka kuna mambo mengi ya kujifunza, zipo kozi za kusoma kwa njia ya mtandao na nyingine za kuingia darasani moja kwa moja,” alisema Enzo.

Taaluma ya utathimini mchezo, alianza kuifanyia kazi katika timu ya Tanzania Prisons msimu ulioisha, akitokea KMC alikokuwa meneja wa timu.

Japo hakutaka kuweka wazi, kuhusu kujiunga na JKT Tanzania, Mwanaspoti linafahamu atakuwa sehemu ya kikosi hicho na ni pendekezo la kocha Hamad Ally aliyefanya naye kazi Prisons na KMC.

Kwa upande wa Rashid Seif (Azam), alisema kozi hizo nchini hazipo, wanasoma kwa njia ya mtandao (online), wakati mwingine kulazimika kwenda nchi ambazo zinapatikana.

“Nimesoma kutoka nchi ya Hispania, nina ngazi ya cheti, ila kwa sasa nasoma nachukua Diploma, njia pekee ya kusoma kwa kuingia darasani ni kwenda nchi husika. Binafsi nasoma kwa njia ya online, pia nasoma Masters Shahada ya Uzamili ya Utawala (Management), kinachowakwamisha Watanzania wengi nadhani ni gharama ni kubwa, kadri unavyoendelea kusoma inaweza ikafika Sh50 milioni,” alisema Seif.

Alisema kilichomshawishi kusomea ni kwa sababu anapenda mpira, akaona taaluma hiyo ni muhimu kwake kuifahamu kwa kina, ili kufanya kazi kwa mapana zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live