Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Acha tumwambie Gamondi

Gamondi Bacca 6972d12 Acha tumwambie Gamondi

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tumuambie tu mapema ili baadaye asije sema tunamsimanga, Gamondi anaifanya Yanga kuwa kama Simba SC, kama ambavyo Robertinho aliua Simba kwenye Kikosi cha Taifa Stars hata Gamondi naye namuona anaenda kuua tena Taifa Stars

Kama Gamondi alicheza mchezo wa nyumbani dhidi ya Al Ahly kwa kujilinda vile, vipi akienda ugenini kucheza na Medeama ambao wamemfunga CR Belouizdad bao3?

Mchezo wa nyumbani unaanza na Bacca, Mwamnyeto, Job, Yao, Lomalisa/Kibabage mwishoni ukamuingiza na Mauya ukamtia Maix, maana yake unataka kulinda home?

Achana na hivyo Gamondi naona kama anataka kuua vipaji kama vya kina Nkane , Farid, Moloko ambao kipindi cha Nabi walikuwa wanapata nafasi ya kusambaza upendo.

Kinachoendelea Gamondi kutuaminisha kwamba wachezaji walio sub Yanga ni wabovu wakati walio wengi ndiyo hao hao alikuwa nao Nabi.

Ule utamaduni wa kila mmoja kupata namba kwenye kikosi cha Yanga kina Ngushi naona unaenda kupotea na anajitengenezea mazingira ya kikosi finyu.

Mwisho wa siku wachezaji watachoka sana kwa kutumika muda mrefu kama kina Kapombe na Zimbwe mwisho wa siku tuanze kuulaum tena uongozi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live