Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Acha maneno, weka mziki wa Mabingwa Ulaya

IMG 5787 Bayern Vs United.jpeg Acha maneno, weka mziki wa Mabingwa Ulaya

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Acha maneno, weka mziki. Pengine hicho ndicho mashabiki wa Manchester United watamwambia kocha wao, Erik ten Hag wakati miamba hiyo ya Old Trafford itakaporusha kete ya pili kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa leo Jumanne. Man United ilikubali kichapo cha mabao 4-3 kutoka kwa Bayern Munich kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi A, hivyo itahitaji ushindi dhidi ya Galatasaray ya Uturuki kuweka hai matumaini yao ya kuvuka kwenye hatua hiyo ya makundi.

Mambo ya Man United yamekuwa hovyo msimu huu, ambapo wikiendi iliyopita ilijikuta ikipoteza mchezo wa nne kwenye Ligi Kuu England katika mechi saba ilizocheza baada ya kuchapwa 1-0 na Crystal Palace. Itakuwaje? Ngoja tuone.

Arsenal baada ya kuichapa PSV mabao 4-0 uwanjani Emirates, itakuwa ugenini kusaka ushindi wa pili kwenye Kundi B itakapokwenda kumenyana na Lens. Arsenal imekuwa kwenye ubora mkubwa sana msimu huu, ikiwa haijapoteza mechi yoyote kwenye Ligi Kuu England hadi sasa. Mechi nyingine ya Kundi B itazikutanisha Sevilla na PSV, ambapo kila timu itajaribu kusaka ushindi wake wa kwanza kwenye mikikimikiki hiyo msimu huu.

Kwenye Kundi A, wababe wengine watakaochuana ni Copenhagen watakaokuwa nyumbani kucheza na Bayern. Mechi ya kwanza Copenhagen ilifungana 2-2 na Galatasaray.

Shughuli pevu itakuwa huko Naples, wakati wenyeji Napoli itakapoikaribisha Real Madrid. Miamba hiyo iliyopangwa Kundi C, kila moja itaingia uwanjani kusaka ushindi wake wa pili, ambapo kwenye mechi za kwanza, Napoli iliichapa Braga 2-1 na Real Madrid iliipiga Union Berlin 1-0. Union Berlin na Braga zitamalizana zenyewe.

Mechi nyingine za usiku wa leo Jumanne, Inter Milan itakuwa nyumbani kucheza na Benfica katika mchezo wa Kundi D, ambapo kila timu itajaribu kusaka ushindi wa kwanza - huku wababe wengine kwenye kundi hilo watakaomalizana wenyewe ni RB Salzburg na Real Sociedad.

Kesho, Jumatatu kutashuhudiwa mechi nane nyingine, ambapo mabingwa watetezi, Manchester City watakuwa ugenini kukipiga na RB Leipzig, huku Crvena zvezda watamaliza ubishi na Young Boys. Kasheshe zito litakuwa kwenye mechi ya FC Porto na Barcelona, wakati Borussia Dortmund itakuwa na kazi nzito mbele ya AC Milan.

Newcastle United itakuwa nyumbani kucheza na Paris Saint-Germain, wakati Atletico Madrid itakuwa nyumbani kucheza na Feyenoord, huku Antwerp itakuwa na kasheshe mbele ya Shakhtar Donetsk na Celtic itamaliza ubishi na Lazio.

Chanzo: Mwanaspoti