Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abuya, Aziz wapewa angalizo

Duke Abuya Mzz.jpeg Yanga yawapa angalizo Abuya na Aziz

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imewapa angalizo wachezaji wake wapya ambao wameonekana kung'ara katika mechi dhidi ya Augsburg ya Ujerumani kuwa makini na sifa zinazotolewa na mashabiki na mitandao ya kijamii kwani zinaweza kuwaharibu na kupoteza ubora wao.

Wachezaji waliosifiwa zaidi katika mchezo huo uliochezwa Jumamosi iliyopita kweye Uwanja wa Mbombela na Yanga kulala kwa mabao 2-1, ni Duke Abuya, Mkenya aliyesajiliwa kutoka Singida Black Stars na Aziz Ambambwile ambaye pia ni mchezaji mpya kutokea Singida Fountain Gate.

Pamoja na kuangukia kichapo hicho, wachezaji hao waliotokea benchi walionyesha viwango vya hali ya juu na kuibadilisha timu kipindi cha pili.

Akizungumza jana kutoka nchini Afrika Kusini ambako timu hiyo ipo kwa michezo kadhaa ya kirafiki ya kimataifa, Meneja wa timu hiyo, Walter Harrison, alisema baada ya mechi hiyo na baadhi ya wachezaji kuonyesha viwango vya juu, wamekuwa wakimwagiwa sifa kemkemu, hasa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandaoya kijamii.

Alisema wamewapa angalizo wachezaji wao akili zao wasizipeleke huko, bali waelekeze kwenye mafunzo ya mwalimu Miguel Gamondi na kufanya kile ambacho kimewaleta Yanga.

"Hatutaki sana wachezaji wetu wapya yawaingie mambo ya kwenye mitandao ya kijamii, hasa ya kusifiwa kwa sababu yanaweza kuwatoa mchezoni, tunachotaka kuhakikisha wanaelekeza nguvu na akili zao kwenye lengo mama la kufanya vema mazoezi na kuiletea timu manufaa.

"Haya yanayoendelea kwenye mitandao yanaweza kuwafanya wakabweteka na baadaye wasifanye vizuri, kwetu sisi hayana umuhimu na hatuyaangalii, tunataka atimize majukumu yake uwanjani, hayo ya 'kutrendi' tunawaachia watu wa mitandaoni," alisema Harrison.

Alisema imetokea mara nyingi kwenye soka la Tanzania, baadhi ya wachezaji wanapopata sifa hasa wanapoingia kwenye klabu kubwa, muda mfupi tu baadaye wanabadilika, hivyo wameanza kuwajenga kisaikolojia ili mambo hayo yasiwaathiri kwenye viwango vyao.

Meneja huyo alisema baada ya mechi hiyo, wachezaji wa Yanga wameendelea na mazoezi, ambapo asubuhi wanafanya ya uwanjani na jioni kwenda 'gym', kabla ya mechi yao ya kesho ya Kombe la Mpumalanga dhidi ya TS Galaxy.

Kuhusu mchezaji Shadrack Boka ambaye aliumia kwenye mchezo huo, alisema anaendelea na matibabu na kama hali itaendelea kama ilivyo basi atapelekwa kwenye vipimo ya uchunguzi zaidi.

Baada ya mechi ya kesho, Yanga itamaliza ziara yake Sauzi, Jumapili itakapocheza dhidi ya kwa Kaizer Chiefs, mechi ya Kombe la Toyota, kwenye Uwanja wa Bloemfontein.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: